هَلۡ يَنظُرُونَ إِلَّا تَأۡوِيلَهُۥۚ يَوۡمَ يَأۡتِي تَأۡوِيلُهُۥ يَقُولُ ٱلَّذِينَ نَسُوهُ مِن قَبۡلُ قَدۡ جَآءَتۡ رُسُلُ رَبِّنَا بِٱلۡحَقِّ فَهَل لَّنَا مِن شُفَعَآءَ فَيَشۡفَعُواْ لَنَآ أَوۡ نُرَدُّ فَنَعۡمَلَ غَيۡرَ ٱلَّذِي كُنَّا نَعۡمَلُۚ قَدۡ خَسِرُوٓاْ أَنفُسَهُمۡ وَضَلَّ عَنۡهُم مَّا كَانُواْ يَفۡتَرُونَ ٥٣
Hal yanzurūna illā ta'wīlahū yawma ya'tī ta'wīluhū yaqūlul-ladhīna nasūhu min qablu qad jā'at rusulu rabbinā bil-haqqi fahal lanā min shufa'ā'a fayashfa'ū lanā aw nuraddu fana'mala ghayral-ladhī kunnā na'malu qad khasirū anfusahum wadalla 'anhum mā kānū yaftarūn
Je, lipo wanalo lingojea isipo kuwa matokeo yake? Siku yatapo fika matokeo yake watasema wale walio kisahau: Kweli Mitume wa Mola Mlezi wetu walileta Haki! Je, tunao waombezi ili watuombee? Au turudishwe ili tufanye yasiyo kuwa yale tuliyo kuwa tukiyafanya? Bila ya shaka wamejikhasiri nafsi zao, na yamewapotea waliyo kuwa wakiyazua. 53
Maelezo ya chini
53 Hakika wao hawaiamini hii Qur'ani, na wala hawangojei ila matokeo ambayo Mwenyezi Mungu ameyabainisha kuwa yatawapata wanayo ikataa! Na Siku yatapofika hayo matokeo, nayo ni Siku ya Kiyama, walio ziacha amri zake na maelezo yake, na wakaghafilika kuwa ni waajibu kuiamini, na hali wakiungama madhambi yao, watasema: Hakika walikuja Mitume kutoka kwa Muumba wetu na Mlezi wetu, wakituitia Haki waliyo tumwa kuileta, nasi tukaikataa! Nao wataulizwa: Je, mnao waombezi wakakuombeeni? Nao hawatowapata! Au, je, watarudishwa tena duniani watende mema? Hawatajibiwa! Wamepoteza vitendo vyao kwa kukhadaika na dunia, na umewapotea ule uzushi wa uwongo wa kudai kuna mungu asiye kuwa Allah, Mwenyezi Mungu.