وَقَالَتۡ أُولَىٰهُمۡ لِأُخۡرَىٰهُمۡ فَمَا كَانَ لَكُمۡ عَلَيۡنَا مِن فَضۡلٖ فَذُوقُواْ ٱلۡعَذَابَ بِمَا كُنتُمۡ تَكۡسِبُونَ ٣٩
Waqālat ūlāhum li ukhrāhum famā kāna lakum 'alaynā min fadlin fadhūqul-'adhāba bimā kuntum taksibūn
Na wa mwanzo wao watawaambia wa mwisho wao: Basi nyinyi pia hamkuwa na ubora kuliko sisi. Basi onjeni adhabu kwa sababu ya mliyo kuwa mkiyachuma 39
Maelezo ya chini
39 Na hapa tena watasema wale walio fuatwa kuwaambia walio fuata: Kutuiga kwenu sisi katika ukafiri na uasi hakukufanyeni nyinyi muwe bora kuliko sisi hata mstahiki kupunguziwa adhabu! Basi Mwenyezi Mungu atawaambia wote: Onjeni adhabu mlio jiletea wenyewe kwa kuwa mlikuwa mkizua ukafiri na uasi!