قَالَ فَبِمَآ أَغۡوَيۡتَنِي لَأَقۡعُدَنَّ لَهُمۡ صِرَٰطَكَ ٱلۡمُسۡتَقِيمَ ١٦
Qāla fabimā aghwaytanī la aq'udanna lahum sirātakal-mustaqīm
Akasema: Kwa kuwa umenihukumia upotofu, basi nitawavizia katika Njia yako Iliyo Nyooka. 16
Maelezo ya chini
16 Kwa kumchukia Adam na kumhusudu alisema: Kwa sababu ya kunihukumia kupotoka na kupotea, nakuapia nitawapoteza wana wa Adam wasiifuate Njia yako Iliyo Nyooka, kwa kutumia kila hila zinazo mkinika.