Surat Al-A'raf, aya 156

7:156

۞ وَٱكۡتُبۡ لَنَا فِي هَٰذِهِ ٱلدُّنۡيَا حَسَنَةٗ وَفِي ٱلۡأٓخِرَةِ إِنَّا هُدۡنَآ إِلَيۡكَۚ قَالَ عَذَابِيٓ أُصِيبُ بِهِۦ مَنۡ أَشَآءُۖ وَرَحۡمَتِي وَسِعَتۡ كُلَّ شَيۡءٖۚ فَسَأَكۡتُبُهَا لِلَّذِينَ يَتَّقُونَ وَيُؤۡتُونَ ٱلزَّكَوٰةَ وَٱلَّذِينَ هُم بِـَٔايَٰتِنَا يُؤۡمِنُونَ ١٥٦

Waktub lanā fī hādhihid-dunyā hasanatan wafil-ākhirati innā hudnā ilayka qāla 'adhābī usību bihī man ashā'u warahmatī wasi'at kulla shay'in fasa'aktubuhā lilladhīna yattaqūna wayu'tūnaz-zakawāta walladhīna hum bi'āyātinā yu'minūn

Na utuandikie mema katika dunia hii na katika Akhera. Sisi tumerejea kwako. (Mwenyezi Mungu) akasema: Adhabu yangu nitamsibu nayo nimtakaye. Na rehema yangu imeenea kila kitu. Lakini nitawaandikia khasa wanao mchamngu, na wanao toa Zaka, na wale ambao wanaziamini Ishara zetu, 156

Maelezo ya chini

156 Na tukadirie hapa duniani maisha mema, na tupate tawfiqi tuweze kut'ii, na Akhera tupate malipo mazuri, na maghfira, na rehema, kwa kuwa sisi hakika tumekwisha rejea kwako na tunatubu kwako. Mola Mlezi wao akawaambia: Adhabu yangu namfikishia nimtakaye katika wasio tubu, na rehema yangu imeenea juu ya kila kitu, na nitawaandikia khasa wale wanao jikinga na ukafiri na maasi katika kaumu yako, na wanao toa Zaka zilio lazimishwa, na wanao sadiki Vitabu vyote vilivyo teremka.