Surat Al-A'raf, aya 151

7:151

قَالَ رَبِّ ٱغۡفِرۡ لِي وَلِأَخِي وَأَدۡخِلۡنَا فِي رَحۡمَتِكَۖ وَأَنتَ أَرۡحَمُ ٱلرَّٰحِمِينَ ١٥١

Qāla rabbighfir lī wali'akhī wa adkhilnā fī rahmatika wa anta arhamur-rāhimīn

(Musa) akasema: Mola Mlezi wangu! Nisamehe mimi na ndugu yangu, na ututie katika rehema yako. Nawe ni Mwenye kurehemu kushinda wote wenye kurehemu. 151

Maelezo ya chini

151 Musa alisema: Ewe Mola wangu Mlezi! Nisamehe kwa haya niliyo mfanyia ndugu yangu kabla sijayajua mambo. Na msamehe ndugu yangu ikiwa kakosea katika kushika pahala pangu kwa vizuri. Na tuingize katika eneo la rehema yako, kwani Wewe ndiwe Mwenye rehema nyingi kushinda wote wenye kurehemu.