Surat Al-A'raf, aya 147

7:147

وَٱلَّذِينَ كَذَّبُواْ بِـَٔايَٰتِنَا وَلِقَآءِ ٱلۡأٓخِرَةِ حَبِطَتۡ أَعۡمَٰلُهُمۡۚ هَلۡ يُجۡزَوۡنَ إِلَّا مَا كَانُواْ يَعۡمَلُونَ ١٤٧

Walladhīna kaddhabū bi'āyātinā waliqā'il-ākhirati habitat a'māluhum hal yujzawna illā mā kānū ya'malūn

Na walio zikanusha Ishara zetu na mkutano wa Akhera a'mali zao zimeharibika. Kwani watalipwa ila kwa yale waliyo kuwa wakiyatenda?. 147

Maelezo ya chini

147 Na walio zikanusha Ishara zetu zilio teremshwa juu ya Mitume wetu kwa ajili ya uwongofu, na wakakanusha kukutana nasi Siku ya Kiyama, wakakataa kufufuliwa na kulipwa, vitendo vyao walivyo kuwa wakitarajia viwafae vitapotelea mbali. Hawatokuta ila malipo ya kufru na maasi waliyo endelea nayo kuyatenda.