وَإِذۡ أَنجَيۡنَٰكُم مِّنۡ ءَالِ فِرۡعَوۡنَ يَسُومُونَكُمۡ سُوٓءَ ٱلۡعَذَابِ يُقَتِّلُونَ أَبۡنَآءَكُمۡ وَيَسۡتَحۡيُونَ نِسَآءَكُمۡۚ وَفِي ذَٰلِكُم بَلَآءٞ مِّن رَّبِّكُمۡ عَظِيمٞ ١٤١
Wa idh anjaynākum min āli fir'awna yasūmūnakum sū'al-'adhābi yuqattilūna abnā'akum wayastahyūna nisā'akum wafī dhālikum balā'um mir rabbikum 'azīm
Na pale tulipo kuokoeni kwa watu wa Firauni walio kupeni adhabu za mwisho wa uovu. Wakiwauwa wavulana wenu, na wakawaacha hai wanawake wenu. Na katika hayo yalikuwa majaribio makubwa kutokana na Mola wenu Mlezi. 141
Maelezo ya chini
141 Kumbukeni alipo kuvueni Mwenyezi Mungu Mtukufu kwa uangalizi wake na watu wa Firauni, walio kuwa wakikuadhibuni ukomo wa adhabu, wakikudhalilisheni muwatumikie katika kazi ngumu, wala hawakukuoneeni huruma kama wanyama, wakiuwa wavulana wenu na wakiwabakisha wasichana ili mzidi kudhoofika kwa wingi wa wanawake! Na katika adhabu za Firauni zilizo kushukieni, na kukuvueni nazo, pana mtihani mkubwa wa Mola wenu Mlezi, wala hapana mfano wake.