وَلَمَّا وَقَعَ عَلَيۡهِمُ ٱلرِّجۡزُ قَالُواْ يَٰمُوسَى ٱدۡعُ لَنَا رَبَّكَ بِمَا عَهِدَ عِندَكَۖ لَئِن كَشَفۡتَ عَنَّا ٱلرِّجۡزَ لَنُؤۡمِنَنَّ لَكَ وَلَنُرۡسِلَنَّ مَعَكَ بَنِيٓ إِسۡرَٰٓءِيلَ ١٣٤
Walammā waqa'a 'alayhimur-rijzu qālū yāmūsad'u lanā rabbaka bimā 'ahida 'indaka la in kashafta 'annar-rijza lanu'minanna laka walanursilanna ma'aka banī isrā'īl
Na ilipo waangukia adhabu wakasema: Ewe Musa! Tuombee kwa Mola wako Mlezi kwa aliyo kuahidi. Ukituondolea adhabu hii hapana shaka tutakuamini, na tutawaachilia Wana wa Israili wende nawe. 134
Maelezo ya chini
134 Katika kuzidi kigeugeu chao kama zinavyo badilika sababu, walikuwa kila ikiwashukia namna yoyote ya adhabu wakisema kwa shida na machungu yanayo wapata: Ewe Musa! Tuombee kwa Mola Mlezi wako, kwa vile alivyo kuahidi kuwa ukimwomba atakupa miujiza na atakuitikia dua, atuondolee adhabu hii. Na sisi tunakuapia kuwa ukituondolea basi bila ya shaka tutakuitikia na tutawaachilia wende nawe Wana wa Israili kama ulivyo taka!