ذَٰلِكَ بِمَا قَدَّمَتۡ أَيۡدِيكُمۡ وَأَنَّ ٱللَّهَ لَيۡسَ بِظَلَّٰمٖ لِّلۡعَبِيدِ ٥١
Dhālika bimā qaddamat aydīkum wa annallāha laysa bizallāmil lil-'abīd
Hayo ni kwa sababu ya yale yaliyo kwisha tangulizwa na mikono yenu, na hakika Mwenyezi Mungu si mwenye kuwadhulumu waja. 51
Maelezo ya chini
51 Na hakika Mwenyezi Mungu si mwenye kuwadhulumu waja wake kwa kuwaadhibu kwa madhambi waliyo yatenda. Bali huo ni uadilifu, kwa sababu hawawi sawa muovu na mwema. Basi kuadhibiwa kwake ni kwa vitendo viovu alivyo vitenda mwenyewe.