Surat Al-Anfal, aya 30

8:30

وَإِذۡ يَمۡكُرُ بِكَ ٱلَّذِينَ كَفَرُواْ لِيُثۡبِتُوكَ أَوۡ يَقۡتُلُوكَ أَوۡ يُخۡرِجُوكَۚ وَيَمۡكُرُونَ وَيَمۡكُرُ ٱللَّهُۖ وَٱللَّهُ خَيۡرُ ٱلۡمَٰكِرِينَ ٣٠

Wa idh yamkuru bikal-ladhīna kafarū liyuthbitūka aw yaqtulūka aw yukhrijūka wayamkurūna wayamkurullāhu wallāhu khayrul-mākirīn

Na walipo kupangia mpango walio kufuru wakufunge, au wakuuwe, au wakutoe. Wakapanga mipango yao, na Mwenyezi Mungu akapanga yake. Na Mwenyezi Mungu ndiye mbora wa mipango. 30

Maelezo ya chini

30 Na kumbuka ewe Nabii, neema za Mwenyezi Mungu zilio juu yako, pale washirikina walipo panga njama kukutia nguvuni - ama wakufunge, au wakuuwe, au wakutoe mji! Hakika walikupangia mipango miovu! Na Mwenyezi Mungu Mtukufu alikupangia utokane na shari yao. Na mpango wa Mwenyezi Mungu ndio wa kheri, na una nguvu zaidi, na ndio wenye kushinda.