Surat Al-Anfal, aya 23

8:23

وَلَوۡ عَلِمَ ٱللَّهُ فِيهِمۡ خَيۡرٗا لَّأَسۡمَعَهُمۡۖ وَلَوۡ أَسۡمَعَهُمۡ لَتَوَلَّواْ وَّهُم مُّعۡرِضُونَ ٢٣

Walaw 'alimallāhu fīhim khayral la asma'ahum walaw asma'ahum latawallaw wwahum mu'ridūn

Na Mwenyezi Mungu angeli jua wema wowote kwao ange wasikilizisha, na lau ange wasikilizisha wangeli geuka wakapuuza. 23

Maelezo ya chini

23 Na Mwenyezi Mungu kwa ilimu yake ya tangu na tangu lau angeli ona ndani yao kuwa, katika hali yao hivi sasa, itakuja patikana kheri yoyote kwao hao kwa nafsi zao, na kwa watu, na kwa Haki, basi angeli wafanya wasikie kusikia kwa kuongoka hata Haki ikaingia akilini mwao. Na hata wangeli isikia na wakaifahamu Haki basi bado wasingeli ifuata. Na mapuuza hayawaachi kwa kuzidiwa na pumbao.