Surat Al-Anfal, aya 10

8:10

وَمَا جَعَلَهُ ٱللَّهُ إِلَّا بُشۡرَىٰ وَلِتَطۡمَئِنَّ بِهِۦ قُلُوبُكُمۡۚ وَمَا ٱلنَّصۡرُ إِلَّا مِنۡ عِندِ ٱللَّهِۚ إِنَّ ٱللَّهَ عَزِيزٌ حَكِيمٌ ١٠

Wamā ja'alahullāhu illā bushrā walitatma'inna bihī qulūbukum waman-nasru illā min 'indillāhi innallāha 'azīzun hakīm

Na Mwenyezi Mungu hakufanya haya ila kuwa ni bishara na ili nyoyo zenu zituwe. Na haupatikani ushindi ila kutoka kwa Mwenyezi Mungu. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye nguvu, na Mwenye hikima. 10

Maelezo ya chini

10 Wala Mwenyezi Mungu Mtukufu hakujaalia huko kukuungeni mkono kwa (Malaika) hizo Roho safi ila ni kuwa ni kukupeni khabari njema, kama bishara kwenu kuwa mtashinda, mpate kutua nyoyo na msonge mbele. Na Mwenyezi Mungu anakusaidieni, na wala ushindi hauji ila kwa msaada wa Mwenyezi Mungu, Mwenye nguvu, Mwenye kushinda, ambaye anaye panga mambo kwa pahala pake kwa mujibu wa ujuzi wake usio pitikiwa na chochote.