وَوَهَبۡنَا لَهُۥٓ إِسۡحَٰقَ وَيَعۡقُوبَ نَافِلَةٗۖ وَكُلّٗا جَعَلۡنَا صَٰلِحِينَ ٧٢
Wawahabnā lahū ishāqa waya'qūba nāfilatan wakullan ja'alnā sālihīn
Naye tukampa Is-haq, na Yaaqub kuwa ni ziada. Na wote tukawajaalia wawe watu wema. 72
Maelezo ya chini
72 Na tukampa Ibrahim mtoto Is-haq, na kutokana na Is-haq tukampa Yaaqubu, zaidi kuliko aliyo taka. Na wote wawili, Is-haq na Yaaqubu tuliwajaalia kuwa ni watu wema.