Surat Al-Anbiya, aya 56

21:56

قَالَ بَل رَّبُّكُمۡ رَبُّ ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَٱلۡأَرۡضِ ٱلَّذِي فَطَرَهُنَّ وَأَنَا۠ عَلَىٰ ذَٰلِكُم مِّنَ ٱلشَّٰهِدِينَ ٥٦

Qāla bar rabbukum rabbus-samāwāti wal-ardil-ladhī fatarahunna wa ana 'alā dhālikum minash-shāhidīn

Akasema: Bali Mola wenu Mlezi ni Mola Mlezi wa mbingu na ardhi ambaye ndiye aliye ziumba. Na mimi ni katika wenye kuyashuhudia hayo. 56

Maelezo ya chini

56 Akasema: Hapana maskhara katika niyasemayo. Bali Mola wenu Mlezi anaye stahiki peke yake kutukuzwa na kuogopwa na kuabudiwa ndiye aliye ziumba mbingu na ardhi, na akazileta bila ya kuwapo mfano wake wa kuigiza. Basi ni haki yake Yeye tu peke yake kuabudiwa. Na mimi kwa haya niyasemayo ni katika wenye hakika ambao hunena wanayo yashuhudia na wanayajua.