إِذۡ قَالَ لِأَبِيهِ وَقَوۡمِهِۦ مَا هَٰذِهِ ٱلتَّمَاثِيلُ ٱلَّتِيٓ أَنتُمۡ لَهَا عَٰكِفُونَ ٥٢
Idh qāla li abīhi waqawmihī mā hādhihit-tamāthīlul-latī antum lahā 'ākifūn
Alipo mwambia baba yake na watu wake: Ni nini haya masanamu mnayo yashughulikia kuyaabudu? 52
Maelezo ya chini
52 Ewe Nabii! Kumbuka pale Ibrahim alipo mwambia baba yake na watu wake kuwaonya juu ya masanamu waliyo kuwa wakishughulikia kuyaabudu: Ni nini haya masanamu ambayo nyinyi mmeshika kuyaabudu?