Surat Al-Anbiya, aya 29

21:29

۞ وَمَن يَقُلۡ مِنۡهُمۡ إِنِّيٓ إِلَٰهٞ مِّن دُونِهِۦ فَذَٰلِكَ نَجۡزِيهِ جَهَنَّمَۚ كَذَٰلِكَ نَجۡزِي ٱلظَّٰلِمِينَ ٢٩

Waman yaqul minhum innī ilāhum min dūnihī fadhālika najzīhi jahannama kadhālika najziz-zālimīn

Na yeyote kati yao atakaye sema: Mimi ni mungu, badala yake, basi huyo tutamlipa malipo yake Jahannamu. Hivyo ndivyo tuwalipavyo wenye kudhulumu. 29

Maelezo ya chini

29 Na miongoni mwa Malaika atakaye sema: Mimi ni mungu wa kuabudiwa badala ya Mwenyezi Mungu, huyo tutamlipa kwa kumtia Jahannamu. Mfano wa malipo hayo tunamlipa kila mwenye kupindukia mipaka ya haki, na wakajidhulumu nafsi zao kwa kudai Ungu na kuingia katika ushirikina.