لَا يُسۡـَٔلُ عَمَّا يَفۡعَلُ وَهُمۡ يُسۡـَٔلُونَ ٢٣
Lā yus'alu 'ammā yaf'alu wahum yus'alūn
Yeye hahojiwi kwa ayatendayo, na wao ndio wanao hojiwa kwa wayatendayo. 23
Maelezo ya chini
23 Yeye Subhanahu hahojiwi kwa anayo yatenda, kwani ni Yeye pekee mwenye utukufu na madaraka, Mwenye hikima na ujuzi. Hakosei katika kutenda chochote. Ni wao ndio watahisabiwa na kuhojiwa kwa wanayo yatenda, kwa kuwa wao hukosea kwa udhaifu wao na ujinga wao na kughilibiwa na matamanio.