Surat Al-Anbiya, aya 19

21:19

وَلَهُۥ مَن فِي ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَٱلۡأَرۡضِۚ وَمَنۡ عِندَهُۥ لَا يَسۡتَكۡبِرُونَ عَنۡ عِبَادَتِهِۦ وَلَا يَسۡتَحۡسِرُونَ ١٩

Walahū man fis-samāwāti wal-ardi waman 'indahū lā yastakbirūna 'an 'ibādatihī walā yastahsirūn

Na ni vyake Yeye tu Mwenyezi Mungu vilivyomo mbinguni na katika ardhi. Na walioko kwake hawafanyi kiburi wakaacha kumuabudu, wala hawachoki. 19

Maelezo ya chini

19 Na ni vya Mwenyezi Mungu peke yake vyote viliomo mbinguni na katika ardhi, kwa kuviumba na kuvimiliki. Basi ni haki Yeye peke yake kuabudiwa. Na Malaika walio karibishwa kwake hawana kiburi cha kuwazuia kumuabudu na kumnyenyekea, wala hawaoni machofu na kunyong'onyea kwa ibada ya mchana na usiku.