Surat Al-An'am, aya 97

6:97

وَهُوَ ٱلَّذِي جَعَلَ لَكُمُ ٱلنُّجُومَ لِتَهۡتَدُواْ بِهَا فِي ظُلُمَٰتِ ٱلۡبَرِّ وَٱلۡبَحۡرِۗ قَدۡ فَصَّلۡنَا ٱلۡأٓيَٰتِ لِقَوۡمٖ يَعۡلَمُونَ ٩٧

Wahuwal-ladhī ja'ala lakumun-nujūma litahtadū bihā fī zulumātil-barri wal-bahri qad fassalnal-āyāti liqawmin ya'lamūn

Na Yeye ndiye aliye kuwekeeni nyota ili mwongoke kwazo katika kiza cha bara na bahari. Hakika tumezichambua Ishara hizi kwa watu wanao jua. 97

Maelezo ya chini

97 Yeye ndiye aliye kufanyieni nyota zikuongozeni kwa zilivyo pangwa mfike mwendako, nanyi mnakwenda kizani usiku, bara au baharini. Hakika Sisi tumezibainisha dalili za rehema yetu, na uwezo wetu, kwa ajili ya watu ambao wanao nufaika kwa ilimu.