وَكَذَّبَ بِهِۦ قَوۡمُكَ وَهُوَ ٱلۡحَقُّۚ قُل لَّسۡتُ عَلَيۡكُم بِوَكِيلٖ ٦٦
Wakaddhaba bihī qawmuka wahuwal-haqqu qul lastu 'alaykum biwakīl
Na watu wako wameikanusha, nayo ni Haki. Sema: Mimi sikuwakilishwa juu yenu. 66
Maelezo ya chini
66 Na kaumu yako wameikanusha Qur'ani, nayo ni Haki ambayo haina cha kukanushwa ndani yake. Ewe Nabii! Waambie: Mimi sikuwekwa kuwa ni muwakilishi wa kukulindeni, na kupima vitendo vyenu na kukulipeni kwavyo. Bali mambo yenu katika hayo yako kwa Mwenyezi Mungu.