قُلۡ مَن يُنَجِّيكُم مِّن ظُلُمَٰتِ ٱلۡبَرِّ وَٱلۡبَحۡرِ تَدۡعُونَهُۥ تَضَرُّعٗا وَخُفۡيَةٗ لَّئِنۡ أَنجَىٰنَا مِنۡ هَٰذِهِۦ لَنَكُونَنَّ مِنَ ٱلشَّٰكِرِينَ ٦٣
Qul man yunajjīkum min zulumātil-barri wal-bahri tad'ūnahū tadarru'an wakhufyatal la in anjānā min hādhihī lanakūnanna minash-shākirīn
Sema: Ni nani anaye kuokoeni katika giza la nchi kavu na baharini? Mnamwomba kwa unyenyekevu na kwa siri, mkisema: Kama akituokoa na haya bila ya shaka tutakuwa miongoni mwa wanao shukuru. 63
Maelezo ya chini
63 Ewe Nabii! Waambie washirikina: Nani anaye kuvueni na vitisho vya bara na baharini vinapo kutokeeni, mkamuaungukia na mkamwomba kwa unyenyekevu wa dhaahiri na wa ndani, mkisema: Tunaapa! Kama ukituvua na vitisho hivi tutakuwa katika wanao kiri fadhila yako, na wanao dumu kukushukuru?