Surat Al-An'am, aya 132

6:132

وَلِكُلّٖ دَرَجَٰتٞ مِّمَّا عَمِلُواْۚ وَمَا رَبُّكَ بِغَٰفِلٍ عَمَّا يَعۡمَلُونَ ١٣٢

Walikullin darajātum mimmā 'amilū wamā rabbuka bighāfilin 'ammā ya'malūn

Na wote wana daraja mbali mbali kutokana na yale waliyo yatenda. Na Mola wako Mlezi si mwenye kughafilika na yale wanayo yatenda. 132

Maelezo ya chini

132 Na kila mtenda kheri au mtenda shari ana daraja yake ya malipo kwa anayo yatenda. Ikiwa kheri atapata kheri, na ikiwa shari basi atapata shari. Na Mwenyezi Mungu Aliye takasika ndiye Muumba, si Mwenye kughafilika na wanayo yatenda. Bali hakika vitendo vyao vimo katika Kitabu kisicho acha dogo wala kubwa ila hulitia hisabuni.