Surat Al-An'am, aya 102

6:102

ذَٰلِكُمُ ٱللَّهُ رَبُّكُمۡۖ لَآ إِلَٰهَ إِلَّا هُوَۖ خَٰلِقُ كُلِّ شَيۡءٖ فَٱعۡبُدُوهُۚ وَهُوَ عَلَىٰ كُلِّ شَيۡءٖ وَكِيلٞ ١٠٢

Dhālikumullāhu rabbukum lā ilāha illā huwa khāliqu kulli shay'in fa'budūhu wahuwa 'alā kulli shay'in wakīl

Huyo ndiye Allah, Mwenyezi Mungu, Mola Mlezi wenu, hapana mungu ila Yeye, Muumba wa kila kitu. Basi muabuduni Yeye tu. Naye ni Mtegemewa wa kila kitu. 102

Maelezo ya chini

102 Huyo aliye sifika kwa sifa za ukamilifu ndiye Allah, Mwenyezi Mungu, Mola Mlezi wenu, ambaye hapana mungu isipo kuwa Yeye, Muumba wa kila kitu vilivyo kuweko, na vitavyo kuwa. Basi ni Yeye tu Mwenye kustahiki kuabudiwa. Basi muabuduni Yeye, na Yeye peke yake ndiye Mwenye kutawala kila kitu na kila jambo. Marejeo yote ni kwake tu.