Surat Al-Ahzab, aya 9

33:9

يَٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ ٱذۡكُرُواْ نِعۡمَةَ ٱللَّهِ عَلَيۡكُمۡ إِذۡ جَآءَتۡكُمۡ جُنُودٞ فَأَرۡسَلۡنَا عَلَيۡهِمۡ رِيحٗا وَجُنُودٗا لَّمۡ تَرَوۡهَاۚ وَكَانَ ٱللَّهُ بِمَا تَعۡمَلُونَ بَصِيرًا ٩

Yā'ayyuhal-ladhīna āmanudhkurū ni'matallāhi 'alaykum idh jā'atkum junūdun fa arsalnā 'alayhim rīhan wajunūdal lam tarawhā wakānallāhu bimā ta'malūna basīrā

Enyi mlio amini! Zikumbukeni neema za Mwenyezi Mungu zilio juu yenu. Pale yalipo kufikilieni majeshi, nasi tukayapelekea upepo, na majeshi msiyo yaona. Na Mwenyezi Mungu anayaona mnayo yatenda. 9

Maelezo ya chini

9 Enyi mlio amini zikumbukeni neema na fadhila za Mwenyezi Mungu zilio juu yenu, pale yalipo kujieni makundi katika Siku ya Handaki. Tukawapelekea upepo mkali wa kimbunga ubaridi, na Malaika ambao nyinyi hamwaoni. Kikawaingia kiwewe katika nyoyo zao. Na Mwenyezi Mungu alikuwa Mwenye kuviona vitendo vyenu, na ukweli wa niya zenu. Basi akaingia kukulindeni.