Surat Al-Ahzab, aya 63

33:63

يَسۡـَٔلُكَ ٱلنَّاسُ عَنِ ٱلسَّاعَةِۖ قُلۡ إِنَّمَا عِلۡمُهَا عِندَ ٱللَّهِۚ وَمَا يُدۡرِيكَ لَعَلَّ ٱلسَّاعَةَ تَكُونُ قَرِيبًا ٦٣

Yas'alukan-nāsu 'anis-sā'ati qul innamā 'ilmuhā 'indallāhi wamā yudrīka la'allas-sā'ata takūnu qarībā

Watu wanakuuliza khabari ya Saa (ya Kiyama). Sema: Ujuzi wake uko kwa Mwenyezi Mungu. Na nini kitakujuvya? Pengine hiyo Saa iko karibu. 63

Maelezo ya chini

63 Watu wanakuuliza lini itasimama Saa ya Kiyama. Waambie hao: Hakika ujuzi wa wakati wake uko kwa Mwenyezi Mungu peke yake. Na nini kitakujuvya? Pengine wakati wa kusimama Saa ya kiyama upo karibu.