وَمَن لَّا يُجِبۡ دَاعِيَ ٱللَّهِ فَلَيۡسَ بِمُعۡجِزٖ فِي ٱلۡأَرۡضِ وَلَيۡسَ لَهُۥ مِن دُونِهِۦٓ أَوۡلِيَآءُۚ أُوْلَٰٓئِكَ فِي ضَلَٰلٖ مُّبِينٍ ٣٢
Wamal lā yujib dā'iyallāhi falaysa bimu'jizin fil-ardi walaysa lahū min dūnihī awliyā'u ulā'ika fī dalālim mubīn
Na wasio mwitikia Mwitaji wa Mwenyezi Mungu basi hao hawatashinda katika ardhi, wala hawatakuwa na walinzi mbele yake. Hao wamo katika upotovu ulio dhaahiri. 32
Maelezo ya chini
32 Na asiye muitikia Mwenyezi Mungu basi hawezi kumshinda Mwenyezi Mungu asimtie mkononi hata akikimbia vipi katika ardhi. Na wala hana isipo kuwa Mwenyezi Mungu wa kumnusuru na kumkinga na adhabu yake. Hao wanao puuza wasimwitikie mwenye kuitia kwa Mwenyezi Mungu wamo katika ubabaishi na dhaahiri wako mbali na Haki.