قَالُوٓاْ أَجِئۡتَنَا لِتَأۡفِكَنَا عَنۡ ءَالِهَتِنَا فَأۡتِنَا بِمَا تَعِدُنَآ إِن كُنتَ مِنَ ٱلصَّٰدِقِينَ ٢٢
Qālū aji'tanā lita'fikanā 'an ālihatinā fa tinā bimā ta'idunā in kunta minas-sādiqīn
Wakasema: Je! Umetujia ili ututenge mbali na miungu yetu? Basi tuletee hayo unayo tuahidi ikiwa wewe ni miongoni mwa wasemao kweli. 22
Maelezo ya chini
22 Kaumu ya Hud walisema kwa kumkanya: Hivyo ndio umetujia ili utuachishe kuwaabudu miungu yetu? Basi tuletee hiyo adhabu ikiwa wewe hakika ni mwenye kusema kweli kwa ahadi hiyo.