وَقَالَ ٱلۡمَلِكُ ٱئۡتُونِي بِهِۦٓ أَسۡتَخۡلِصۡهُ لِنَفۡسِيۖ فَلَمَّا كَلَّمَهُۥ قَالَ إِنَّكَ ٱلۡيَوۡمَ لَدَيۡنَا مَكِينٌ أَمِينٞ ٥٤
Waqālal-maliku'tūnī bihī astakhlishu linafsī falammā kallamahū qāla innakal-yawma ladaynā makīnun amīn
Basi mfalme akasema: Mleteni kwangu, awe wangu mwenyewe khasa. Basi alipo msemeza alinena: Hakika wewe leo umekwisha tamakani kwetu na umeaminika. 54
Maelezo ya chini
54 Usafi wa Yusuf ulipo dhihiri kwa mfalme, aliazimu amwite. Akawatuma watu wake wamlete awe wake yeye mwenyewe wa kumsafia niya. Basi alipo hudhuria na yakapita baina yao mazungumzo, mfalme akaathirika na utukufu wa Yusuf kwa usafi wa nafsi yake, na ubora wa rai zake! Akamwambia: Sasa wewe kwangu utakuwa na cheo cha hishima kilicho thibiti. Na wewe ni muaminifu kwangu ninaye kuamini.