Surat Yusuf, aya 52

12:52

ذَٰلِكَ لِيَعۡلَمَ أَنِّي لَمۡ أَخُنۡهُ بِٱلۡغَيۡبِ وَأَنَّ ٱللَّهَ لَا يَهۡدِي كَيۡدَ ٱلۡخَآئِنِينَ ٥٢

Dhālika liya'lama annī lam akhunhu bil-ghaybi wa annallāha lā yahdī kaydal-khā'inīn

Hayo ni apate kujua ya kwamba mimi sikumfanyia khiyana nyuma yake; na ya kwamba Mwenyezi Mungu haziongoi hila za makhaini. 52

Maelezo ya chini

52 Haya mimi naungama kwa kweli ninayo itoa, apate kuwa na yakini Yusuf kuwa mimi sikuchukua fursa ya kuto kuwepo alipo kuwa gerezani nikaendelea na khiyana, na nikamdhulumu kwa kumtuhumu. Na kwa kuwa hakika Mwenyezi Mungu haijaalii kufanikiwa mipango ya makhaini.