Surat Yusuf, aya 17

12:17

قَالُواْ يَٰٓأَبَانَآ إِنَّا ذَهَبۡنَا نَسۡتَبِقُ وَتَرَكۡنَا يُوسُفَ عِندَ مَتَٰعِنَا فَأَكَلَهُ ٱلذِّئۡبُۖ وَمَآ أَنتَ بِمُؤۡمِنٖ لَّنَا وَلَوۡ كُنَّا صَٰدِقِينَ ١٧

Qālū yā'abānā innā dhahabnā nastabiqu wataraknā yūsufa 'inda matā'inā fa akalahudh-dhi'bu wamā anta bimu'minil lanā walaw kunnā sādiqīn

Wakasema: Ewe baba yetu! Hakika tulikwenda kushindana na tukamwacha Yusuf penye vitu vyetu. Basi mbwa mwitu akamla. Lakini wewe hutuamini ijapo kuwa tunasema kweli. 17

Maelezo ya chini

17 Wakasema: Ewe baba yetu! Sisi tulikwenda kushindana kupiga mishale na kwenda mbio, na tukamwacha Yusuf kwenye vitu vyetu avilinde. Mbwa mwitu akamla, na sisi tuko mbali tumeshughulika na mashindano! Na wewe hutusadiki tunayo yasema, ijapokuwa tunasema haki na kweli!