وَنَجِّنَا بِرَحۡمَتِكَ مِنَ ٱلۡقَوۡمِ ٱلۡكَٰفِرِينَ ٨٦
Wanajjinā birahmatika minal-qawmil-kāfirīn
Na utuokoe kwa rehema yako na watu makafiri. 86
Maelezo ya chini
86 Wakamwomba Mola wao Mlezi wakisema: Kwa vile ulivyo tumiminia neema na rehema, na kwa wingi wa rehema yako unayo sifika nayo, tuokoe na hawa watu wanao kataa, wenye kudhulumu.