Surat Yunus, aya 84

10:84

وَقَالَ مُوسَىٰ يَٰقَوۡمِ إِن كُنتُمۡ ءَامَنتُم بِٱللَّهِ فَعَلَيۡهِ تَوَكَّلُوٓاْ إِن كُنتُم مُّسۡلِمِينَ ٨٤

Waqāla mūsā yāqawmi in kuntum āmantum billāhi fa'alayhi tawakkalū in kuntum muslimīn

Na Musa alisema: Enyi watu wangu! Ikiwa nyinyi mmemuamini Mwenyezi Mungu, basi mtegemeeni Yeye, ikiwa nyinyi ni Waislamu. 84

Maelezo ya chini

84 Ama Musa aliwaambia Waumini kwa kuwawasa na kuwashajiisha: Enyi watu wangu! Ikiwa Imani imekwisha ingia nyoyoni mwenu kwa kumsafishia niya Mwenyezi Mungu, basi msimwogope yeyote mwenginewe. Nanyi msalimishie Yeye mambo yenu yote, na mtegemeeni Yeye, na muwe na yakini mwishoe atakunusuruni, ikiwa nyinyi mmethibiti katika Uislamu.