Surat Yunus, aya 36

10:36

وَمَا يَتَّبِعُ أَكۡثَرُهُمۡ إِلَّا ظَنًّاۚ إِنَّ ٱلظَّنَّ لَا يُغۡنِي مِنَ ٱلۡحَقِّ شَيۡـًٔاۚ إِنَّ ٱللَّهَ عَلِيمُۢ بِمَا يَفۡعَلُونَ ٣٦

Wamā yattabi'u aktharuhum illā zannan innaz-zanna lā yughnī minal-haqqi shay'an innallāha 'alīmu bimā yaf'alūn

Na wengi wao hawafuati ila dhana tu. Na dhana haifai kitu mbele ya haki. Hakika Mwenyezi Mungu anajua yote wanayo yatenda. 36

Maelezo ya chini

36 Wengi wa washirikina hawafuati katika itikadi zao ila dhana potovu zisio kuwa na dalili zozote! Na kwa jumla, dhana haifidi kitu, wala haiwezi kuwa ni badala ya kuijua Haki, na khasa ikiwa dhana yenyewe ni ya kuzua tu, kama hizi dhana za washirikina. Na hakika Mwenyezi Mungu anayajua vyema wayafanyayo wakuu wa ukafiri na wafuasi wao, naye atawalipa kwa hayo.