Surat Yunus, aya 18

10:18

وَيَعۡبُدُونَ مِن دُونِ ٱللَّهِ مَا لَا يَضُرُّهُمۡ وَلَا يَنفَعُهُمۡ وَيَقُولُونَ هَٰٓؤُلَآءِ شُفَعَٰٓؤُنَا عِندَ ٱللَّهِۚ قُلۡ أَتُنَبِّـُٔونَ ٱللَّهَ بِمَا لَا يَعۡلَمُ فِي ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَلَا فِي ٱلۡأَرۡضِۚ سُبۡحَٰنَهُۥ وَتَعَٰلَىٰ عَمَّا يُشۡرِكُونَ ١٨

Waya'budūna min dūnillāhi mā lā yadurruhum walā yanfa'uhum wayaqūlūna hā'ulā'i shufa'ā'unā 'indallāhi qul atunabbi'ūnallāha bimā lā ya'lamu fis-samāwāti walā fil-ardi subhānahū wata'ālā 'ammā yushrikūn

Nao, badala ya Mwenyezi Mungu, wanaabudu wasio wadhuru wala kuwanufaisha,na wanasema: Hawa ndio waombezi wetu kwa Mwenyezi Mungu! Sema: Je! Mnamwambia Mwenyezi Mungu asiyo yajua ya katika mbingu wala katika ardhi? Subhanahu wa Taa'la! Ametakasika na ametukuka na hao wanao mshirikisha naye. 18

Maelezo ya chini

18 Na hawa washirikina wanao mzulia Mwenyezi Mungu kuwa ana washirika, wanaabudu masanamu ya upotovu. Hayawadhuru wala hayawanufaishi. Na wanasema: Masanamu haya yatatuombea kwa Mwenyezi Mungu Siku ya Akhera! Ewe Mtume! Waambie: Hivyo nyinyi mnamwambia Mwenyezi Mungu kuwa ana washirika ambao hawajui, la katika mbingu wala katika ardhi? Mwenyezi Mungu ametakasika na kuwa na washirika, na yote mnayo zua kwa kuwaabudu hao washirika.