Surat Yunus, aya 109

10:109

وَٱتَّبِعۡ مَا يُوحَىٰٓ إِلَيۡكَ وَٱصۡبِرۡ حَتَّىٰ يَحۡكُمَ ٱللَّهُۚ وَهُوَ خَيۡرُ ٱلۡحَٰكِمِينَ ١٠٩

Wattabi' mā yūhā ilayka wasbir hattā yahkumallāhu wahuwa khayrul-hākimīn

Na wewe fuata yanayo funuliwa kwako kwa wahyi. Na vumilia mpaka Mwenyezi Mungu ahukumu, na Yeye ndiye mbora wa mahakimu. 109

Maelezo ya chini

109 Ewe Mtume! Thibiti juu ya Dini ya Haki. Na fuata wahyi ulio teremshiwa, nawe uwe na subira kwa maudhi yanayo kufika kwa ajili ya Njia ya Da'wa (Wito), mpaka Mwenyezi Mungu ahukumu baina yako na wao, kwa vile alivyo kuahidi kuwa atawapa ushindi Waumini, na watahizika makafiri. Na Yeye ndiye mbora wa mahakimu.