Surat Hud, aya 92

11:92

قَالَ يَٰقَوۡمِ أَرَهۡطِيٓ أَعَزُّ عَلَيۡكُم مِّنَ ٱللَّهِ وَٱتَّخَذۡتُمُوهُ وَرَآءَكُمۡ ظِهۡرِيًّاۖ إِنَّ رَبِّي بِمَا تَعۡمَلُونَ مُحِيطٞ ٩٢

Qāla yāqawmi arahtī a'azzu 'alaykum minallāhi wattakhadhtumūhu warā'akum zihriyyan inna rabbī bimā ta'malūna muhīt

Akasema: Enyi watu wangu! Kwani jamaa zangu ni watukufu zaidi kwenu kuliko Mwenyezi Mungu? Na Yeye mmemueka nyuma ya migongo yenu! Hakika Mola wangu Mlezi ni Mwenye kuyazunguka yote mnayo yatenda. 92

Maelezo ya chini

92 Akasema Shua'ibu: Enyi watu wangu! Hivyo jamaa zangu ndio wanastahiki kufanyiwa wema kuliko Mwenyezi Mungu. Wao mnawakumbuka, na mkataka kunifanyia jamala mimi kwa ajili yao. Lakini Yeye mmemsahau na mkamfanya kama kitu kilicho tupiliwa mbali nyuma ya migongo yenu! Hakika Mola Mlezi wangu ni Mwenye kuyazunguka yote mnayo yafanya kwa kuyajua, hapana linalo fichikana kwake katika vitendo vyenu, na atakuhisabieni kwavyo hata ikiwa nyinyi mtasahau.