Surat Hud, aya 86

11:86

بَقِيَّتُ ٱللَّهِ خَيۡرٞ لَّكُمۡ إِن كُنتُم مُّؤۡمِنِينَۚ وَمَآ أَنَا۠ عَلَيۡكُم بِحَفِيظٖ ٨٦

Baqiyyatullāhi khayrul lakum in kuntum mu'minīna wamā ana 'alaykum bihafīz

Alivyo kubakishieni Mwenyezi Mungu ndiyo bora kwa ajili yenu, ikiwa nyinyi ni Waumini. Wala mimi siye mlinzi wenu. 86

Maelezo ya chini

86 Kidogo kinacho kuzidieni katika mali ya halali aliyo kuruzukuni Mwenyezi Mungu ni bora kwenu kuliko chungu ya mali mnayo yakusanya kwa njia ya haramu, ikiwa nyinyi kweli mnamuamini Mwenyezi Mungu, na mnaepuka aliyo kukatazeni. Basi jipimeni nafsi zenu, na mumuangalie Mola wenu Mlezi. Mimi si mlinzi wenu wa kuchunga vitendo vyenu na kukupimieni.