قَالُواْ يَٰصَٰلِحُ قَدۡ كُنتَ فِينَا مَرۡجُوّٗا قَبۡلَ هَٰذَآۖ أَتَنۡهَىٰنَآ أَن نَّعۡبُدَ مَا يَعۡبُدُ ءَابَآؤُنَا وَإِنَّنَا لَفِي شَكّٖ مِّمَّا تَدۡعُونَآ إِلَيۡهِ مُرِيبٖ ٦٢
Qālū yāsālihu qad kunta fīnā marjuwwan qabla hādhā atanhānā an na'buda mā ya'budu ābā'unā wa innanā lafī shakkim mimmā tad'ūnā ilayhi murīb
Wakasema: Ewe Swaleh! Hakika kabla ya haya ulikuwa unatarajiwa kheri kwetu. Je, unatukataza tusiwaabudu waliyo kuwa wakiwaabudu baba zetu? Na hakika sisi tuna shaka na wasiwasi kwa hayo unayo tuitia. 62
Maelezo ya chini
62 Wakasema: Ewe Swaleh! Hakika wewe ulikuwa kwetu mtu wa kutarajiwa mema, na kupendwa, na kutukuzwa katika nyoyo zetu, kabla ya haya unayo tuitia! Hivyo unatutaka tuache ibada waliyo kuwa wakiabudu baba zetu na tuliyo izoea sisi na wao? Hakika sisi tuna shaka na huo wito wako wa kumuabudu Mwenyezi Mungu Mmoja. Haya ni mambo ya kukutilia shaka na dhana mbovu wewe na huo wito wako!