Surat Hud, aya 60

11:60

وَأُتۡبِعُواْ فِي هَٰذِهِ ٱلدُّنۡيَا لَعۡنَةٗ وَيَوۡمَ ٱلۡقِيَٰمَةِۗ أَلَآ إِنَّ عَادٗا كَفَرُواْ رَبَّهُمۡۗ أَلَا بُعۡدٗا لِّعَادٖ قَوۡمِ هُودٖ ٦٠

Wa utbi'ū fī hādhihid-dunyā la'natan wayawmal-qiyāmati alā inna 'ādan kafarū rabbahum alā bu'dal li'ādin qawmi hūd

Na wakafuatishiwa laana katika dunia hii na Siku ya Kiyama. Basi tambueni mtanabahi! Hakika kina A'adi walimkufuru Mola wao Mlezi. Na tambueni mtanabahi kuwa hakika waliangamizwa kina A'adi, kaumu ya Huud. 60

Maelezo ya chini

60 Kwa hivyo wakastahiki kutoka kwa Mwenyezi Mungu, na Malaika, na watu wote kupata laana ya hapa duniani, na laana ya kuwafuatia Siku ya Kiyama. Basi na atanabahi kila mwenye kuijua khabari ya A'adi kwamba hao kina A'adi waliikataa neema ya Muumba wao kwao, wala hawakuishukuru kwa kumuamini Yeye peke yake. Kwa hivyo ndio wakawa wanastahili wafukuzwe kwenye rehema ya Mwenyezi Mungu, na wateremshiwe maangamizo makali! Hebu zingatieni maangamizo yao kwa kumkadhibisha Huud!