Surat Hud, aya 57

11:57

فَإِن تَوَلَّوۡاْ فَقَدۡ أَبۡلَغۡتُكُم مَّآ أُرۡسِلۡتُ بِهِۦٓ إِلَيۡكُمۡۚ وَيَسۡتَخۡلِفُ رَبِّي قَوۡمًا غَيۡرَكُمۡ وَلَا تَضُرُّونَهُۥ شَيۡـًٔاۚ إِنَّ رَبِّي عَلَىٰ كُلِّ شَيۡءٍ حَفِيظٞ ٥٧

Fa in tawallaw faqad ablaghtukum mā ursiltu bihī ilaykum wayastakhlifu rabbī qawman ghayrakum walā tadurrūnahū shay'an inna rabbī 'alā kulli shay'in hafīz

Na ikiwa watarudi nyuma, basi mimi nimekwisha kufikishieni niliyo tumwa kwenu. Na Mola wangu Mlezi atawaleta watu wengine badala yenu, wala nyinyi hamumdhuru kitu Yeye. Hakika Mola wangu Mlezi ni Mwenye kuhifadhi kila kitu. 57

Maelezo ya chini

57 Na mkiukataa wito wangu, basi kukataa kwenu hakunidhuru kitu. Na mwisho mbaya utakuwa wenu. Kwani mimi nimekwisha kufikishieni ujumbe aliyo nituma Mwenyezi Mungu kwenu. Na sina jukumu ila kufikisha tu. Na Mwenyezi Mungu atakuangamizeni nyinyi, na awalete watu wengine wachukue majumba yenu na mali yenu! Na nyinyi hamumdhuru kitu chochote Yeye kwa kukataa kwenu kumuabudu! Hakika Mola wangu Mlezi ni Mlinzi wa kila kitu, Mwenye kujua kila kitu. Basi hapana katika mtendalo linalo fichikana kwake, wala haghafiliki kukutieni nguvuni.