Surat Hud, aya 48

11:48

قِيلَ يَٰنُوحُ ٱهۡبِطۡ بِسَلَٰمٖ مِّنَّا وَبَرَكَٰتٍ عَلَيۡكَ وَعَلَىٰٓ أُمَمٖ مِّمَّن مَّعَكَۚ وَأُمَمٞ سَنُمَتِّعُهُمۡ ثُمَّ يَمَسُّهُم مِّنَّا عَذَابٌ أَلِيمٞ ٤٨

Qīla yānūhuhbit bisalāmim minnā wabarakātin 'alayka wa'alā umamim mimmam ma'aka wa umamun sanumatti'uhum thumma yamassuhum minnā 'adhābun alīm

Ikasemwa: Ewe Nuhu! Shuka kwa salama itokayo kwetu, na baraka nyingi juu yako na juu ya watu walio pamoja nawe. Na zitakuwapo kaumu tutakazo zistarehesha, na kisha zitashikwa na adhabu chungu itokayo kwetu. 48

Maelezo ya chini

48 Akaambiwa kwa wahyi: Ewe Nuhu! Teremka nchi kavu kutokana na hiyo Safina ya uwokovu, salama usalimina, kwa amani itokanayo kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu, na baraka nyingi zitokazo kwa Mwenyezi Mungu juu yako na juu ya hao walio pamoja nawe, ambao watakuja kuwa mataifa mbali mbali baada yako. Na baadhi yao watapata baraka ya Imani na ut'iifu, na baadhi yao watakuwa watu wanao itaka starehe ya dunia, na watapata starehe yake bila ya kuit'ii Haki. Kisha Siku ya Kiyama itawapata adhabu chungu na kali.