قَالَ يَٰنُوحُ إِنَّهُۥ لَيۡسَ مِنۡ أَهۡلِكَۖ إِنَّهُۥ عَمَلٌ غَيۡرُ صَٰلِحٖۖ فَلَا تَسۡـَٔلۡنِ مَا لَيۡسَ لَكَ بِهِۦ عِلۡمٌۖ إِنِّيٓ أَعِظُكَ أَن تَكُونَ مِنَ ٱلۡجَٰهِلِينَ ٤٦
Qāla yānūhu innahū laysa min ahlika innahū 'amalun ghayru sālihin falā tas'alni mā laysa laka bihī 'ilmun innī a'izuka an takūna minal-jāhilīn
Akasema: Ewe Nuhu! Huyu si katika ahali zako. Mwendo wake si mwema. Basi usiniombe jambo usio na ujuzi nalo. Mimi nakuwaidhi usije ukawa miongoni mwa wajinga. 46
Maelezo ya chini
46 Allah Subhanahu akasema: Hakika huyo mwanao si katika ahali zako. Kwani yeye kwa ukafiri wake na mwendo wake pamoja na makafiri amekata makhusiano baina yako na yeye. Naye ametenda vitendo visio vyema. Kwa hivyo amekuwa si katika wewe. Nawe usitake jambo usilo lijua, kuwa ndilo au silo. Wala usende kufuata huruma zako. Na mimi nakuongoza njia ya Haki ili usiwe katika wajinga ukasahau kwa huruma zako Hakika iliyo thibiti!