Surat Hud, aya 101

11:101

وَمَا ظَلَمۡنَٰهُمۡ وَلَٰكِن ظَلَمُوٓاْ أَنفُسَهُمۡۖ فَمَآ أَغۡنَتۡ عَنۡهُمۡ ءَالِهَتُهُمُ ٱلَّتِي يَدۡعُونَ مِن دُونِ ٱللَّهِ مِن شَيۡءٖ لَّمَّا جَآءَ أَمۡرُ رَبِّكَۖ وَمَا زَادُوهُمۡ غَيۡرَ تَتۡبِيبٖ ١٠١

Wamā zalamnāhum walākin zalamū anfusahum famā aghnat 'anhum ālihatuhumul-latī yad'ūna min dūnillāhi min shay'il lammā jā'a amru rabbika wamā zādūhum ghayra tatbīb

Na Sisi hatukuwadhulumu, lakini wao wenyewe wamejidhulumu. Na miungu yao waliyo kuwa wakiiomba badala ya Mwenyezi Mungu haikuwafaa kitu ilipo kuja amri ya Mola wako Mlezi. Na hiyo miungu haikuwazidishia ila maangamizo tu. 101

Maelezo ya chini

101 Wala Sisi hatukuwadhulumu kwa vile tulivyo wateketeza; lakini wamejidhulumu wenyewe kwa kufuru zao, na kuacha kumuabudu Mwenyezi Mungu, na kuleta uharibifu katika nchi. Kwa hivyo miungu yao waliyo kuwa wakiiabudu badala ya Mwenyezi Mungu haikuweza kuwakinga na hilaki, wala haikuwafaa kitu ilipo kuja amri ya Mola wako Mlezi, ewe Nabii! Na kushikilia kwao kuabudu masanamu hakukuwazidishia ila hilaki na upotovu!