Surat Fussilat, aya 52

41:52

قُلۡ أَرَءَيۡتُمۡ إِن كَانَ مِنۡ عِندِ ٱللَّهِ ثُمَّ كَفَرۡتُم بِهِۦ مَنۡ أَضَلُّ مِمَّنۡ هُوَ فِي شِقَاقِۭ بَعِيدٖ ٥٢

Qul ara'aytum in kāna min 'indillāhi thumma kafartum bihī man adallu mimman huwa fī shiqāqi ba'īd

Sema: Mnaonaje! Ikiwa haya yanatoka kwa Mwenyezi Mungu, nanyi ikawa ndio mmeyakataa, ni nani aliye potea zaidi kuliko aliye katika upinzani wa mbali? 52

Maelezo ya chini

52 Ewe Muhammad! Waambie: Hebu nambieni; ikiwa hii Qur'ani imetoka kwa Mwenyezi Mungu nanyi mkawa mnaikataa, basi nani aliye kuwa mbali mno na Ukweli kuliko huyo aliye kinyume na Haki?