Surat Fatir, aya 11

35:11

وَٱللَّهُ خَلَقَكُم مِّن تُرَابٖ ثُمَّ مِن نُّطۡفَةٖ ثُمَّ جَعَلَكُمۡ أَزۡوَٰجٗاۚ وَمَا تَحۡمِلُ مِنۡ أُنثَىٰ وَلَا تَضَعُ إِلَّا بِعِلۡمِهِۦۚ وَمَا يُعَمَّرُ مِن مُّعَمَّرٖ وَلَا يُنقَصُ مِنۡ عُمُرِهِۦٓ إِلَّا فِي كِتَٰبٍۚ إِنَّ ذَٰلِكَ عَلَى ٱللَّهِ يَسِيرٞ ١١

Wallāhu khalaqakum min turābin thumma min nutfatin thumma ja'alakum azwājan wamā tahmilu min unthā walā tada'u illā bi'ilmihī wamā yu'ammaru mim mu'ammarin walā yunqasu min 'umurihī illā fī kitābin inna dhālika 'alallāhi yasīr

Na Mwenyezi Mungu amekuumbeni kutokana na udongo. Kisha kwa tone la manii. Kisha akakufanyeni mwanamume na mwanamke. Na mwanamke yeyote hachukui mimba, wala hazai, ila kwa ilimu yake. Na wala hapewi umri mwenye umri mrefu, wala hapunguziwi katika umri wake, ila yamo hayo katika Kitabu. Hakika hayo ni mepesi kwa Mwenyezi Mungu. 11

Maelezo ya chini

11 Na Mwenyezi Mungu amekuumbeni kutokana na udongo. Kwani ndivyo hivyo alivyo muumba baba yenu Adam. Kisha akakuumbeni kutokana na tone ya manii, nayo ni maji yanayo miminwa katika tumbo la uzazi, nayo pia ni katika chakula kinacho toka kwenye udongo. Kisha akakufanyeni waume na wake. Wala mwanamke hachukui mimba, wala hazai ila kwa ujuzi wa Mwenyezi Mungu Mtukufu. Wala hauongezwi umri wa mtu yeyote, wala haupunguzwi ila husajiliwa katika Kitabu. Hakika hayo kwa Mwenyezi Mungu ni sahali, mepesi.