وَتَرَى ٱلۡمَلَٰٓئِكَةَ حَآفِّينَ مِنۡ حَوۡلِ ٱلۡعَرۡشِ يُسَبِّحُونَ بِحَمۡدِ رَبِّهِمۡۚ وَقُضِيَ بَيۡنَهُم بِٱلۡحَقِّۚ وَقِيلَ ٱلۡحَمۡدُ لِلَّهِ رَبِّ ٱلۡعَٰلَمِينَ ٧٥
Wataral-malā'ikata hāffīna min hawlil-'arshi yusabbihūna bihamdi rabbihim waqudiya baynahum bil-haqqi waqīlal-hamdu lillāhi rabbil-'ālamīn
Na utawaona Malaika wakizunguka pembeni mwa Kiti cha enzi cha Mwenyezi Mungu, wakimtakasa na kumsifu Mola wao Mlezi. Na patahukumiwa baina yao kwa haki na patasemwa: Sifa zote njema ni za Mwenyezi Mungu, Mola Mlezi wa viumbe vyote! 75
Maelezo ya chini
75 Na utaona, ewe mwenye kuona, Malaika wakiizunguka A'rshi, wakimtakasa Mwenyezi Mungu na kila upungufu, kwa utakaso unao fuatana na kumhimidi Muumba wao na Mlezi wao, na akapambanua baina ya viumbe vyote kwa uadilifu, na ulimwengu wote ukatamka kwa kusema: Sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, Mola Mlezi wa viumbe vyote.