Surat Az-Zumar, aya 71

39:71

وَسِيقَ ٱلَّذِينَ كَفَرُوٓاْ إِلَىٰ جَهَنَّمَ زُمَرًاۖ حَتَّىٰٓ إِذَا جَآءُوهَا فُتِحَتۡ أَبۡوَٰبُهَا وَقَالَ لَهُمۡ خَزَنَتُهَآ أَلَمۡ يَأۡتِكُمۡ رُسُلٞ مِّنكُمۡ يَتۡلُونَ عَلَيۡكُمۡ ءَايَٰتِ رَبِّكُمۡ وَيُنذِرُونَكُمۡ لِقَآءَ يَوۡمِكُمۡ هَٰذَاۚ قَالُواْ بَلَىٰ وَلَٰكِنۡ حَقَّتۡ كَلِمَةُ ٱلۡعَذَابِ عَلَى ٱلۡكَٰفِرِينَ ٧١

Wasīqal-ladhīna kafarū ilā jahannama zumaran hattā idhā jā'ūhā futihat abwābuhā waqāla lahum khazanatuhā alam ya'tikum rusulum minkum yatlūna 'alaykum āyāti rabbikum wayundhirūnakum liqā'a yawmikum hādhā qālū balā walākin haqqat kalimatul-'adhābi 'alal-kāfirīn

Na walio kufuru wataongozwa kuendea Jahannamu kwa makundi. Mpaka watakapo ifikia itafunguliwa milango yake, na walinzi wake watawaambia: Kwani hawakukujilieni Mitume miongoni mwenu wakikusomeeni Aya za Mola wenu Mlezi na kukuonyeni mkutano wa siku yenu hii? Watasema: Kwani! Lakini limekwisha thibiti neno la adhabu juu ya makafiri. 71

Maelezo ya chini

71 Na makafiri watahimizwa kwenda kwa nguvu kuendea Jahannamu kwa makundi makundi. Na hata watapo fika milango yake itafunguliwa, na walinzi wake watawaambia kwa kuwakebehi: Kwani hawakuja kwenu Wajumbe kutoka kwa Mwenyezi Mungu wa jinsi yenu, wakikusomeeni Aya za Mola wenu Mlezi, na wakakuhadharisheni na mkutano wenu huu? Makafiri watasema kwa kukiri: Kwani! Walitujia Mitume. Lakini neno la adhabu limekwisha wajibikia juu ya makafiri, kwa kuwa wao wamekhiari ukafiri kuliko Imani.