فَأَصَابَهُمۡ سَيِّـَٔاتُ مَا كَسَبُواْۚ وَٱلَّذِينَ ظَلَمُواْ مِنۡ هَٰٓؤُلَآءِ سَيُصِيبُهُمۡ سَيِّـَٔاتُ مَا كَسَبُواْ وَمَا هُم بِمُعۡجِزِينَ ٥١
Fa asābahum sayyi'ātu mā kasabū walladhīna zalamū min hā'ulā'i sayusībuhum sayyi'ātu mā kasabū wamā hum bimu'jizīn
Basi ukawasibu uovu wa waliyo yachuma. Na wale walio dhulumu miongoni mwa hawa utawasibu uovu wa waliyo yachuma vile vile. Nao si wenye kushinda. 51
Maelezo ya chini
51 Yakawasibu makafiri walio tangulia malipo ya madhambi ya vitendo vyao, na madhaalimu miongoni mwa hawa wanao semezwa hivi sasa yatawapata vile vile malipo ya madhambi ya vitendo vyao. Wala hawa hawataiepuka adhabu.