Surat At-Tawbah, aya 70

9:70

أَلَمۡ يَأۡتِهِمۡ نَبَأُ ٱلَّذِينَ مِن قَبۡلِهِمۡ قَوۡمِ نُوحٖ وَعَادٖ وَثَمُودَ وَقَوۡمِ إِبۡرَٰهِيمَ وَأَصۡحَٰبِ مَدۡيَنَ وَٱلۡمُؤۡتَفِكَٰتِۚ أَتَتۡهُمۡ رُسُلُهُم بِٱلۡبَيِّنَٰتِۖ فَمَا كَانَ ٱللَّهُ لِيَظۡلِمَهُمۡ وَلَٰكِن كَانُوٓاْ أَنفُسَهُمۡ يَظۡلِمُونَ ٧٠

Alam ya'tihim naba'ul-ladhīna min qablihim qawmi nūhin wa'ādin wathamūda waqawmi ibrāhīma wa ashābi madyana wal-mu'tafikāti atathum rusuluhum bil-bayyināti famā kānallāhu liyazlimahum walākin kānū anfusahum yazlimūn

Je, hazikuwafikia khabari za walio kuwa kabla yao - kaumu ya Nuhu, na A'ad, na Thamud, na kaumu ya Ibrahim, na watu wa Madyana, na miji iliyo pinduliwa chini juu? Mitume wao waliwafikia kwa hoja zilizo wazi. Basi Mwenyezi Mungu hakuwa mwenye kuwadhulumu, walakini wao walikuwa wakijidhulumu wenyewe. 70

Maelezo ya chini

70 Basi je, hawazingatii wanaafiki na makafiri hali ya walio watangulia katika kaumu ya Nuhu na A'ad na Thamud na kaumu ya Ibrahim na kaumu ya Shuaib na kaumu Lut'? Mitume wa Mwenyezi Mungu waliwajia na hoja zilizo wazi wazi kutokana na Mwenyezi Mungu, na wakawakanusha na wakawakataa! Mwenyezi Mungu akawashika kila mmoja wao kwa dhambi zake, na akawateketeza wote! Wala Mwenyezi Mungu hakuwadhulumu, lakini walizidhulumu wenyewe nafsi zao kwa ukafiri wao, na uasi wao kumuasi Mwenyezi Mungu, na wakastahiki peke yao kupata adhabu. Basi wao ndio wanao jidhulumu wenyewe.