لِيَجۡزِيَهُمُ ٱللَّهُ أَحۡسَنَ مَا عَمِلُواْ وَيَزِيدَهُم مِّن فَضۡلِهِۦۗ وَٱللَّهُ يَرۡزُقُ مَن يَشَآءُ بِغَيۡرِ حِسَابٖ ٣٨
Liyajziyahumullāhu ahsana mā 'amilū wayazīdahum min fadlihī wallāhu yarzuqu man yashā'u bighayri hisāb
Ili Mwenyezi Mungu awalipe bora ya waliyo yatenda, na awazidishie katika fadhila zake. Na Mwenyezi Mungu humruzuku amtakaye bila ya hisabu. 38
Maelezo ya chini
38 Na malipo ya vitendo vyao ni kulipwa sawa sawa kwa ubora wa malipo kwa vitendo vyao vyema, na watapata fadhila kwa kupewa zaidi kuliko wanavyo stahiki. Kwani Yeye Subhanahu ni Mkunjufu wa fadhila, humpa amtakaye katika waja wake wema kipao kikubwa, asichoweza mtu kukihisabu wala wenye kuhisabu hawawezi kukisia.